Nilitaka mmalize nyie kwanza kuongea sasa ni zam yangu, Nilihoji Mie katika Post ya Diamond Kuonekana kwenye harusi ya Peter wa P’Square, Je Kaka kaalikwa au kavamia maana kivazi kilienda kinyume na waalikwa. sasa leo imedhihirika ukweli kuwa bwana huyu alivamia baada ya bwana harusi mwenyewe kumkana live kupitia Radio mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili Ya show yao kubwa iliyofanyika Leader Club Jumamosi na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Katika Mahojiano hayo yaliofanyika East Africa Radio Mtangazaji alimuuliza Peter Ambaye ndio alikuwa bwana harusi wiki moja iliyopita wakati anafanya ndoa ya kimila kama Kuna Mwanamuziki kutoka Tanzania Alimualika? Bahati mbaya kwa Diamond Peter alishangazwa na uwepo wake na kuonyesha kutomfahamu msanii huyo hata baada ya kuchezewa wimbo wake. kwa lugha ingine tunaweza sema Diamond Alivamia Harusi Hiyo Na ndio maana hata kivazi chake kilileta utata kutokana na kutokuwa na Card ambayo ingemuonyesha Angalau Dress Code
Haikuwa Kitu Kibaya Diamond kuhudhuria Harusi Hiyo ila kwasababu kwetu ni msanii mkubwa lazima tuhoji na tujue maendeleo yake na kafikaje lakini pia kutokana na harusi yenyewe aliohudhuria kuwa ya wasanii wa kubwa Afrika kila mmoja alikuwa na shauku ya Kufahamu Lolote. So kwasababu Diamond ndio alipost Picha Hizo basi angesema mapema ilikuwaje kuwaje akawepo leo aibu hii isingemkuta
Mbwembwe zikizidi mara ingine zinaweza kukushusha
Diamond Washabiki wako wanakupenda sana sana usiwaangushe basi