Chini) Baada ya kuwa wapenzi kwa miaka mitatu, Jason Derulo amemaliza mahusiano yake na muimbaji wa kike mkali wa ngoma ya “No Air” kwa njia ya simu wiki iliyoisha, Derulo amepokea malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki kuhusiana na mahusiano yake na pia alikutana na waandishi wa habari kujieleza.
Alikubali alikubali kuachana na Jordin Sparks kupitia simu kwa sababu hakuwepo mjini. Jordin alichukua simu na kwenda mbele anamwambia Kathie Lee Gifford “Niko fresh, nimesoma nukuu na ilisomeka “ Pindi inapotokea kitu ambacho hukutegemea katika maisha yako au unawaza kitu fulani kinatokea, sema play twist na usonge mbele”.
(Chini) Taylor Swift ameweka wazi kwamba Joe Jonas alimuacha vibaya kwa simu aliyopigiwa na maongezi ya muda mfupi sana mwaka 2008. Muimbaji huyo wa “Last Kiss” alimwambia Ellen DeGeneres, kutengena kwao ilikuwa kama, historia, nadhani kwa haraka, niliangalia sehemu ya kupigia simu, ilikuwa ni kama sekunde 27.
Hiyo imekuwa rekodi, akiongelea rekodi, Swift amesema amekuwa akiandika nyimbo nyingi zikiwa zinamsukumo kutoka katika maisha yake ya muziki. Lakini Joe anasisitiza kwamba “We are never ever getting back together” is not about him.
(Chini) Si utani, Mchekeshaji Russell Brand alimpa mke wake Katy Perry miezi 14, “Ni mwanaume mwenye akili na nilikuwa mahabani nae sina hili wala lile toka tulipooana” “Tuseme sijawahi kusikia kutoka kwake alinitumia ujumbe ukisema alikuwa ananipa talaka mimi Desemba 31, 2011” Katy Perry aliliambia Vogue.
(Chini) Muigizaji Minnie Driver aligundua hakuwa mpenzi waMatt Damon kwa wakati ule ule ikiwa ni sehemu ya dunia nzima, wakati alipoonekana kwenye show ya Oprah 1998 Muigizaji huyo alisema alikuwa hana mpenzi na hiyo ilikuwa ni habari kwa Driver, ambaye alikuwa kwa mema muigizaji huyo na alimtafuta kwa miezi saba iliyopita, Ni kwa bahati mbaya kwamba Matt aliendaa kwenye show ya Oprah. Aliliambia Los Angeles Times, inaonekana kama ilionekana kama ni sehemu nzuri ya kutangazia dunia kwamba walikuwa hawana mahusiano tena ambapo ilionekana sio njia nzuri ya kufanya hivyo.
(Chini) Carrie Underwood pia alikubali yeye na mpenzi wake Chase Crawford waliachana kwa SMS mwaka 2008.
(Chini) Iliripotiwa Britney Spears alikatisha ndoa yake iliyodumu kwa miaka miwili na dancer wake Kevin Federline kwa meseji mwaka 2006.
(Chini) Ukiaongelea kuhusu mahusiano yaliyoongelewa sana, ni pale Sylvester alipoachana na Jennifer Flavin, aliachana nae kwa ujumbe uliofikwisha kwake na Federal Express kampuni ya kufikisha mizigo sehemu mbalimbali. Alimtumia makaratasi yenye kurasa sita akiwa ameandika kwa mkono kwa kutumia kalamu, mwanamitindo huyo Jennifer Flavin aliiambia People mwaka 1994.
(Chini) Bill Bob Thornton kuachana kwake kwa mwaka 2002 na muigizaji Laura Dern kweli ilikuwa mbaya sana, Dern ambae aliishi Los Angeles, aligundua kwamba mpenzi wake mzuri kwa miaka 3 alimuacha na kwenda kwa Angelina Jolie tena ile kinoma noma. Aliondoka kwenda kazini kwa ajili ya kufanya filamu na wakati akiwa huko, mpenzi wake alioa na hajawahi kusikia chochote kutoka kwake tena, muigizaji huyo aliiambia Talk Magazine.
(Chini) Mahusiano kati ya mastaa wenye usiri Isabelle Adjani na Daniel Day-Lewis ghafla yalifika mwisho mwaka 1996, lakini sio kwa fax kama ripoti fulani zilivyosema. Akiwa kama mshindi wa Oscar muigizaji huyo alienda clinic huko Paris kuangali afya yake, Muigizaji huyo wa Kifaransa alimwambia alikuwa mjamzito, haikuwa kwa fax kama ilivyoripotiwa “ Penzi langu kwake lilikuwa la uhakika lakini nadhani haikuwa hivyo kwa mwenzangu, hatukuonana tena, hajawahi kuniambia kwamba it was over, natamani angeniambia napenda vitu vinavyoeleweka” alisema Adjani.