Meya wa jiji la Arusha ametakiwa kuonyesha utofauti na wakati wa halmashauri hiyo ilipokuwa chini ya CCM.
Hayo yamesemwa na Mwenyenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe alipokutana na Meya wa jiji la Arusha, Mhe. Kalist Lazaro, na weheshimiwa wabunge na madiwani kutoka Arusha.
Amewataka kuonyesha tofauti kubwa wakati halmashauri hiyo ikiwa chini ya CCM, kwa kuleta maendeleo na kununi vyanzo vipya vya mapato ili kuinua uchumi wa jiji hilo.
“Tukae tushirikiane na wananchi wote katika kuleta maendeleo, hakikisheni mnatetea wananchi, wameamini wakawapa dhamana ya kuwaongoza wakiamini nyie ndio watetezi wao, shirikianeni nao, sikilizeni kero zao, ili muweze kuzitatua kwa pamoja kwa kuwashirikisha ” amesema Mhe. Mbowe.
Aidha amempongeza Meya kwa kuongeza mapato kutoka Shilingo milioni 800 hadi Bilioni 1.5 kwa mwezi, amemtaka waendelee kubuni miradi na kukusanya kodi kikamilifu lakini kuangalia kodi zile ambazo hazimbani mwananchi ili kila mmoja aweze kufaidika sio kuacha wengine wakiminywa.
Kuhusu Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA), Mhe. Mbowe amesisitiza isidhaniwe kwamba ni utani amesisitiza lengo lipo pale pale, Maandamano na Mikutano nchi nzima ifikapo Septemba Mosi, 2016, Maandamano yapo kwa mujibu wa Katiba ambayo Rais aliapa kuilinda na kuitetea, Chama cha siasa uhai wake upo kwenye mikutano ya kisiasa.
Amesisitiza maandalizi yanaendelea vizuri, kuanzia ngazi ya Taifa,Kanda, Mkoa, Wilaya, Kata na Kaya.
“Haiwezekani nchi ikaongozwa kwa amri za mtu mmoja, hakuna mtu aliye juu ya sheria, sheria lazima zifuatwe, sheria tumezitunga wenyewe lazima tuziheshimu, hivyo hapa mbele ya waandishi muwapashe habari Watanzania adhma yetu ipo pale pale” ameongeza.