
Watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia tawi la Benki Ya Habib lililopo makutano ya barabara ya uhuru na livingstone Jijini Dar Es Salaam na kupora kiasi cha takribani shilingi bilioni moja kabla ya kutoweka
uporaji huo umetokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo gari aina ya Noah lilifika eneo hili na watu watano kuteremka mmoja akiwa maevalia sare za police na mwingine akiwa na Radio Call Huku wawili wakibeba mifuko ya rambo kama vile wanapleka Fedha katika Benki hiyo na baadaye kuwaweka chini ya uliunzi wafanya kazi wote pamoja na walinzi wawili na kuanza kupora Fedha kujaza mifuko waliyokwenda nayo
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam CP Suleiman Kova amesema mara baada ya uporaji huo watuhumiwa hao walitoroka bila hata majirani na watu wengine kugundua tukio hilo.
Jeshio la Polisi linamshikilia Meneja wa tawi hilo Daniel Matemba kwa kushindwa kuchukua hatua kwa kubonyeza alama ya hatari wakati tukio la uporaji likiendelea huku akishuhudia kwa mbali akiwa katika Ofisi yake, pamoja na walinzi waliokuwa zam
Kamanda Kova ametaja kiasi kilichoibiwa kuwa ni shilingi milioni 792 pamoja na dola za kimarekani 181,885 ambapo kamishna Kova ameomba ushirikiano wa wananchi kwa yeyote ambaye atakuwa na taarifa zinazowezesha kusaidia kuwatia mbaroni watuhumiwa kuziwasilisha polisi, Aidha ametangaza zawadi ya shilingi milioni mia moja kwa atakaesaidia kuwasilisha taarifa hizo.
