Mke Wa Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr.Gharib Bilali, Mama Asha Bilal Amependezesha Zaidi usiku wa kanga za kale ulioandaliwa na Mbunifu wa mavazi wa siku nyingi Asia Idariuos Wa Khamsin katika Hotel ya kimataifa ya Serena Iliyopo Jijini Dar Es Salaam
Mama Asha Bilal Alikuwa mgeni Rasmi Katika usiku huo uliopambwa na burudani mbali mbali kutoka katika kundi la Mashauzi Classic, na Ngoma za utamaduni huku kukinogeshwa na wanamitindo waliovalia vazi la kanga waliopita jukwaani katika maumbo tofauti tofauti na si yale ya mwili Mwembamba  tuliouzoea
Wabunifu Wakubwa Tanzania kama Mustafa Hassan Ali walionyesha mavazi yao katika mitindo ya kanga huku kukiwa na wabunifu chipukizi pia ambao walipewa nafasi Pia
Picha Za Mavazi ya wabunifu hao zitafuata hivi punde, usibonyeze kidude