Msanii memba wa kundi maarufu linapatina Dodoma Chamber Squad limezidi kupuputika baada ya kuondokewa na msanii mwingine Mez B baada ya Ngwair kufariki mwaka juzi.
Mez B ambaye jina lake halisi ni Moses Bushagama alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Chamber Squad lililotamba na wasanii kama Mangwea (Marehemu), Dark Master na Noorah.
Mez B amefariki siku ya Ijumaa 20/2/2015 akiongea
kupitia Dala Dala Beats ya Magic FM moja kwa moja kutoka Dodoma Dj Tass aliongea na ndugu wa Mez B ambae alisema Mez B alikuwa akisumbuliwa na homa toka mwaka jana Desemba ndipo alikwenda Dodoma ambako ndipo mama yake anapoisha. Baba yake Mez alifariki siku nyingi wakati Mez B akiwa mdogo.
Msiba upo nymbani kwao eneo la Kisasa mkoani Dodoma.
Kwa mwaka huu wa 2015 ni msiba mwingine ambao unatikisa tasnia ya muziki baada ya baba yake Dully Sykes Ebby Sykes kufariki.
Ngoma kali za Mez B zilizompa umaarufu ni pamoja na “Kama Vipi” akiwa na Ray C, Kikuku, Nimekubali na nyingine nyingi.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.