
Ilikuwa ni kitu cha kutisha wakati umati uliokuwa chini ya ghorofa walipomuona mtoto akiwa sehemu ya hatari katika ghorofa ya tano akining’inia katika kibaraza (balcony) cha ghorofa hiyo huko nchini Brazil.
Mhudumu mmoja alikuwa akipita akasikia mtoto analia ndipo alipowaita wateja waje waone nao wakaanza kutafuta msaada.
Taarifa kupitia ninemsn.com zinasema mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu inaaminika alipanda kwenye kiti ili achungulie chini ndipo alipokwama.
Baadae aliokolewa kutoka sehemu hiyo ya hatari na Bruno Teixeira ambae alisema mama wa mtoto huyo alikuwa amelala ndani wakati wote tukio hilo likienda
“Tulipomuona mtoto huyo ananing’inia tulikimbia bila hata kuangalia na tulipofika kwenye nyumba hiyo mlango ulikuwa wazi na mlango wa kuelekea kibarazani (balcony) alipo mtoto ulikuwa umefungwa na mama wa mtoto huyo alikuwa amelala, yeye ndiye aliyetakiwa angalie maisha ya mtoto wake”
alisema Bruno.
