
Muigizaji maarufu wa nchini Afrika Kusini lesego Motsepe Maarufu kama Letti Matabane Aliyekua anaigiza Tamthilia Ya Isidingo iliyokuwa maarufu hapa Tanzania ikiwa inaonyeshwa na Channel ya ITV amefariki Dunia leo huko Afrika Kusini baada ya kuugua kwa muda mrefu ugojwa wa Ukimwi
Lesego (Letti) Amekutwa amefariki Nyumbani kwake leo kutokana na taarifa iliyotolewa na familia yake Letti alikutwa amekufa Nyumbani kwake RandBurg Afrika Kusini baada ya kukutwa na kaka yake akiwa amefariki
Taarifa Za uchunguzi zinasema Letti amekufa katika kifo cha kawaida tu cha maradhi mida ya saa Saba Mchana akiwa kwenye umri wa miaka 39
Muigizaji huyo amekuwa akiishi na Virusi Vya Ukimwi Tangu Mwaka 1998
Letti amefariki akiwa ni balozi wa maswala ya Ukimwi Nchini Mwake Tangu alipojitangaza Rasmi

1 Comment
Chozi limenidondoka .nilimpenda sana huyu dada.. Hata alipokufa kwa igizo niliumia but sasa ndio nimeumia zaidi