
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 38 kujeruhiwa kati yao 14 vibaya baada ya mgagari matatu waliyokuwa wakisafiria kugongana mawili uso kwa uso huku jingine likijaribu kukwepa ajali katika eneo la Bwawani barabara kuu ya Morogoro – Dar es SalaamWilaya Bagamoyo mkoani Pwani..
Baadhi ya mashuuda wakiwemo majeruhi walionusurika kifo katika ajali hiyo ambaao baadhi yao wamekimbizwa kupatiwa huduma ya kwanza katika Zahanati ya magereza Bwawani wamezungumzia kuhusiana na namna walivyobaini ajali hiyo huku mgannga wa zahanati ya sekondari ya magereza bwawani Lazaro Mdeka akikiri kupokea majeruhi 38 na 14 hali zao ni mbaya na wamekimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro kwa matibabu..,
