
Taarifa za Ghafla mtandao wa burudani nchini Kenya, Msanii wa kike kutoka Kenya Amani, amesema kiwanda cha muziki wa Uganda ni kikubwa ukilinganisha na Kenya, wasanii wa Uganda wajivunie vyombo vyao vya habari alieleza.
Mwanamuziki wa muziki wa reggae Bebe Cool alikuwa msanii wa kwanza kupinga kupewa nafasi kubwa kwa muziki wa Nigeria na Afrika ya kusini nchini Uganda, malalamiko yake alielekeza kwa madjs, kama unakumbuka vita kati ya Bebe Cool na Dj Bekaay na baadhi ya watangazaji wa redio kama Fat Boy.
“Nchi kama Uganda na vyombo vyake vya habri vinatoa nafasi kwa asilimia 90 kwa kucheza muziki wa Uganda na hiyo ndio sababu muziki wao uko juu yetu, Hiyo ni kwa sababu wanacheza muziki wao sana, unapocheza muziki wako sana, kiasi fulani inapelekea kukua kwa kiwanda cha muziki na kukua zaidi” alisema Amani
“Vyombo vyetu vinacheza muziki wetu sio zaidi ya asilimia 60%”.
Mkali huyo wa ngoma ya “Kiboko Changu” anaongeza kwamba wanamuziki wa Kenya wanajulikana zaidi nje ya Kenya kuliko nchini kwao na hiyo ni sababu wanakuwa wakigombea tunzo mbalimbali zaidi ya Tanzania na Uganda.
