Ndege moja ya shirika la ndege la British Airways imelazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea kwa choo
Ndege hiyo ya BA ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo bwana Abhishek Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa
kijamii wa Twitter kuwa ”Amini usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu
kugundua kuwa harufu mbaya inatokea kwenye choo ya ndege hiyo.”
Yamkini rubani wa ndege hiyo aliwaita msimamizi wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo tukang’amua kuwa kulikuwa na tashwishi katika safari yetu”Sachdev alinukuliwa na gazeti moja.
”mara tukaelezwa na rubani kuwa harufu mbaya ndani ya ndege hiyo inatokea kwenye choo kichafu na kuwa ilikuwa ni ya kinyesi”
”Kufikia wakati huo ilikuwa ni takriban nusu saa tangu tupae angani kwa hivyo tukalazimika kurejea Dubai”
Shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa usumbufu wowote kwa abiria wake
”Ajabu ni kuwa hakukuwa na ndege mbadala ya kuturejesha London kwa hivyo ikatubidi kusubiri kwa zaidi ya saa 15 .
hata hivyo walitupeleka hotelini tukapumzika usiku kucha”
Mwakilishi wa ndege hiyo Greg James, Sarah, aliiambia Radio 1 kuwa hilo halikuwa swala la kufanyiwa utani kwani ukiwa ndani ya ndege ni tishio kubwa kwa afya ya rubani na abiria kwa jumla.
”Ndani ya ndege huwa kunautupu wa hewa kwa hivyo asili mia 50 ya hewa inayotumika ni ileile kwa hivyo
harufu mbaya ingeathiri vibaya afya ya abiria ndio sababu ndege hiyo haikuwa na budi ila kurejea iliisafishwe”.
Hata hivyo shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa usumbufu wowote kwa abiria wake walioathirika siku hiyo.
BBC