Juhudi za kimataifa zinaendelea kutafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia iyokuwa ikielekea Beijing nchini China na kupotea baharini ikiwa na abiria 239,
Ndege hiyo iliyopotea aina Boeing 777 ilkuwa na abiria wapatao 239 pamoja na wafanyakazi wa ndege Shirika la ndege la Malaysia limesema ndege hiyo namba MN370 ilipotea majira ya saa 8:40 kwa saa Malaysia siku ya Ijumaa baada ya kuondoa Kuala Lumpur.
Baadhi ya watu ambao ndugu zao wambo ndani ya ndege hiyo wakiwa katika hali ya kukata tamaa kama ndugu zao watapatikana wakiwa hai
Jeshi la Malaysia limesema kikosi cha pili cha helikopta na Meli kimetumwa kwenye eneo la tukio lakini hata hivyo hakuna chochote kilichoonekana katika hatua za awali za utafutaji wa ndege hiyo…
Waziri wa Usafiri wa Malaysia amesema hakuna taarifa za zozote za kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo
“Tunafanya kila linalowezekana ndani ya uwezo wetu kujua ndege hiyo ilipo,” Hishammuddin Hussein amewaambia waandishi wa habari katika mji Kuala Lumpur