Juma mosi iliopita Muigizaji kutoka NoolyWood Omotola Jalade na mume wake Matthew walisherehekea miaka 17 ya ndoa yao huku pia ikiwa ni sikukuu ya kuzaliwa ya Mume wake. Ndoa ambayo ilifungwa kiserekali mwaka 1996 na kimilia ilifungwa mwaka 2001.
Omotola akiwa na mume wake
Omotola alikutana na mumewe katika umri wa miaka 16 ambapo mumewe huyo alitaka kumuoa kwa kipindi hicho hicho lakini mama yake Omotola aliwashauri kusubiri angalau mpaka afikishe miaka 18, Ambapo hatimae Omotola akaolewa akiwa katika umri huo.
Mume wa Omotola na watoto wao wa kike
Omotola Jalade mwenye umri wa miaka miaka 35 sasa alioisherehekea mwezi wa pili mwaka huu huko Atlanta
Marekani alipokua anatengeneza kipindi chake cha “THE REAL OMOSEXY” Amefanikiwa kuwa na watoto wanne wakike na wakiume na Anayafurahia maisha
Omotola anasema watu wengi wanashangaa yeye kuolewa katika umri huo lakini kwakwe si jambo la ajabu, pia anasema mafanikio ya ndoa yao kufikisha umri huo yanatokana na kuaminiana, kuheshimiana na kuwa na upendo wa dhati kati yao.
Mume wa Omotola na watoto wao wa kiume alie kushoto na huyo wa kulia walivyo sasa
Jambo lingine la tofauti kidogo ambalo labda Omotola alilisema ni kwamba yeye na mume wake hawapendi kuwa na marafiki sana na kwamba marafiki ni wao wenyewe wawili na kwamba hakuna anaemzungumzia mwenzie kwa watu au wawe marafiki au wazazi au watu wowote kwani wao lao ni moja na huelezana wao wenyewe kwahiyo mawasiliano yanawaweka karibu zaidi na hakuna mtu kati yao anaeweza sema lolote juu yao kwasababu hawa mshirikishi mtu maisha yao ya ndani.
Kutokana na ukamavu huo katika ndoa Jarida moja la huko Nigeria OK lieitaja na kuifananisha ndoa ya Omotola kama ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle au ndoa ya wanamuziki Jay Z na Beyonce.
Omotola ni muigizaji wa NollyWood huku mumewe akiwa ni Rubani wa Ndege
wanawake wengi tumekua tukiamini kuwa kuolewa na kuzaa ni kuisha kama misemo ya mjini ilivo (ukizaa umekwisha). SIO KWELI! ukweli ni kwamba tunajipotosha wenyewe na kuzaa si uzee wala si kwisha ni wewe mwenyewe kujali afya na mwili wako na namna ya kujenga mwili wako kwa mazoezi mara baada ya kujifungua
Tazama hiyo picha ya Omotola hivyo ndivyo alivyo sasa akiwa na uzao wa watoto 4, jenga picha ya mwanamke aliekata tamaa ya maisha baada ya kuzaa idadi hiyo ya watoto? au hata mmoja tu. eti ukimuuliza NIMEZAA? na ngombe afanye nini lol.
wake up woman, msiwape sababu wanaume kwenda njee ya ndoa zenu kwa kigezo cha manyama uzembe. amfanye akose sababu ili aibu iwe yake.