
Ikiwa ni usiku wa pili (usiku wa kuamkia leo)katika reality show ndani ya jumba la Big Brother Africa mwaka huu lilipewa jina la ‘The chace’ mambo mengi mapya yameanza kuonekana kwa washiriki ambao wameanza kufahamiana.
Katika hali ambayo mara nyingi haikwepeki hasa wanapokutana wanawake warembo na wanaume watanashati, scene za mapenzi zimeanza kuonekana katika Diamond house inayoongozwa na mtanzania Fezza Kessy (Head of house) ….
‘Bolt’ , mshiriki kutoka Sierra Leone na Betty ambae ni mshiriki kutoka Ethiopia walipata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuvuka mstari wa urafiki wa kawaida wakati washiriki wengine wakiwa wamelala ndani ya jumba la Kessy
Betty na Bolt..
Bolt alisikika akimuambia Betty ‘let’s do it” lakini mwanadada Betty aliyeonekana kuwa hoiii kwa kipindi hicho alikua hana jinsi baada ya akili kumjia kuwa kamera zipo On kwa ajili yao,
Betty ambae yuko nominated pasipo yeye kufahamu, sasa yeye na Bolt ndio waliothibitishwa kuwa couple ya kwanza, japo hatima ya mahusiano yao huenda ikawa hatarini kwa kuwa jumapili hii kura za watazamaji zitaamua hatima ya Betty kuendelea kuwa katika jumba hilo au kurudi Ethiopia.

2 Comments
Are they prohibited to do sex in the house?
Add Your Comment Mambo Vipi Watu Wangu Wa Arusha Na Bongo Kwa Ujumla