
Ni kama amegonga vichwa vya habari kibao duniani kwa muda usiopungua mwezi mmoja, kwanza alimwaga meneja wake ambaye ni Jermaine Dupri na sasa aingia ndani ya ndoa akamwaga na Nick Cannon ambaye ni mume wake, sijui ni stress za kutofanya vizuri albamu yake ya Me, Iam Mariah hayo sio majibu ila najaribu tu kujiuliza.
Mariah Carey na Nick Cannon walitengana mwezi Mei kwa sasa wanaishi tofauti kila mtu kwake, taarifa zinaeleza kwamba wanasheria wanaoshughulikia talaka hiyo wamekuwa wakikubaliana jinsi ya kuzigawa mali za wawili hao lakini suala la talaka lishakamilika.
Chanzo kimoja mabcho kipo karibu na wawili hao kimesema kwamba Mariah na Nick wamekuwa wakiishi nyumba tofauti huko New York toka Mwezi Mei. Huwa anakwenda kuwaona watoto na hicho ndo kikubwa ambacho kinawafanya wawasiliane.
Chanzo hicho kinaeleza kwamba Nick Cannon alionekana kwenye kipindi cha redio cha Big Boy show mwezi Machi hapo ndipo ilipokuwa mwanzo wao kutengana. Nick alicheza mchezo wa Big Boy, aliambiwaa ataje watu maarufu aliowahi kutembea nao, Nick aliwataja lakini chanzo hicho kilieleza kwamba kilimchukiza Mariah zaidi na baada ya kusikia kwamba Nick alishatembea na Kim Kardshian.
Taarifa zinaendelea kueleza kwamba Mariah alikuwa mbali kwa kwa wiki kadhaa, akihisi kufanyiwa kitu ambacho si sawa kwa binadamu na mahusiano hayo hayakutengenezwa tena, taarifa ziliendelea kueleza kwamba mambo yalikuwa mabaya zaidi Nick alipoongea na Howard Stern na kusema Mariah yeye ndo hakati tamaa mambo yaishe.
Mariah Carey anahisi kwamba Nick amemtelekeza na kinachomfanya apate hasira ni kwamba swala hilo linamfanya awe mbali na watoto wake.
Kwa upande wa Nick tunaambiwa kwamba anahisi kwamba Mariah amekuwa awezekani kwa sababu amezungukwa na yes men… Anasema Mariah hawezi kuhandle pale anapogoma kukubaliana nae.
.Nick anasema Mariah anamuharibia kuhusu ethic za kazi yake na toka 2011 Nick ametengeneza dola milioni 75 kwa ajili ya familia.
Huyu baba nae katika kutaja watu aliotembea nao siangegoma tu, check sasa kama Lil Wayne alikuwa anataka amchukue Christina Milan anaona haifai tena, lazima waliotajwa katika list hii watachukia watachukia wakisikia hii kwa sababu itawaharibia mambo huko waliko.
