Kijana mmoja wa Kicanada mwanamitindo mwenye umri wa miaka 24 anaeitwa Vin Los amechora tatoos 24 kwenye uso wake na maneno yanayojulikana duniani na kwa lugha zao, taarifa kutoka kwake zinasema anataka kuwa mtu anayejulikana zaidi duniani, aliiambia Vice.
“Nataka kuwa kitu cha kuangaliwa na watu, kitu ambacho kitakuwa na matokeo, kila mtu ananiona anajiuliza “Kwa nini maarufu? Masiha yangu yatakuaje? Ipo wazi, nitaenda youtube nitasikiliza ngoma zote zilizofanya vizuri na nitachukua maneno kutoka katika nyimbo hizo, Top of the world imetoka kwenye wimbo wa Cataracs pia ni kitu nataka, watu wengi wananiuliza siogopi kama siku moja nitajutia, kama ningekuwa mtu wa kusitasita sidhani kama nitaandika kwenye uso wangu” Alisema kijana huyo…
Ni kijana mzuri tu lakini ameamua kufanya hivyo bila hizo tatoo anapendeza lakini ndo hivyo ametaka kuwa mtu maarufu dunainai ajulikane.