Ikiwa ni Ahadi Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh, Dr Jakaya Mrisho Kikwete Kwa Wasanii Wa Tanzania Kuwaletea wataalam wa mambo ya burudani Duniani Ili kutoa somo kwa wasanii waweze kujua namna wenzao walivypfika mbali
Hatimae baada Ya Kukutana na waandishi wa habari, kuzindua kitabu chake pamoja na sinema yake ya Think like a Man 2, Mtangazaji wa kituo cha E Intertainment Terrence J Jana Tarehe 14 July aliongoza semina ya wasanii wa tanzania katika nyanja tofauti akiwa na jopo lake aliloongozana nalo katika ukumbi wa mikutano wa B.O.T jijini Dar Es Salaam
Terence J na ujumbe wake walitoa elimu ya kutosha kwa wasanii namna ya kuweza kufanya sanaa zao kufika mbali na kuwaingizia kipato kwa stahili inayotakiwa
Wasanii Walipata Fursa ya kushare yao na wageni hao ambao walionekana kubobea na kuwa na uzoefu mkubwa katika maswala ya sanaa kwa ujumla
Pamoja na Terence j pia palikuwa na David Banner Rapper Na Producer, Chaka Zulu Manager wa Msanii Luda Criss na Ravi Mfanya biashara, kwa pamoja kila mmojana na nafasi yake alielezea namna wasanii wanavyoweza kutumia nafasi walizonazo kusonga mbele na kupata mafanikio
Picha Za Semina
Terence JTerence J Na Ujumbe WakeDavid Banner Na RaviChaka Zulu Na David Banner
Ruge Mutahaba
Seven