Miss Tanzania 2001 na Mwanamitindo wa kimataifa Millen Happiness magese Ametoa msaada wa kujenga vyumba vyumba vya shule na kugawa madawati katika shule ya msingi huko mtwara vijijini eneo a mji mwema.
Hiyo ilikuwa ni ahadi yake tangu alipokuwa na taji la mrembo wa Tanzania kwa mwaka huo wakati akifanya shughuli za kijamii baada ya kutembelea huko na kukuta watoto wakiwa wanasoma katika vyumba vibovu vya madarasa na kuketi chini
cha kushangaza tangu mwaka huo na mpaka aliporudi tena mwaka jana kwa ajili ya kuanzisha mradi huo alikuta kile kile alichokiacha mwaka 2001 ndipo alipoamua kutia nguvu zaidi na hatimae kufanikiwa kwa kiasi chake mwaka huu
Mwanamitindo huyo ameshare picha za tukio hilo katika mtandao wake wa Picha (INSTAGRAM) na kuonekana kuhamasisha watu wengine kuwa na moyo wa kujitoa na kuchangia kwa namna moja ama nyingine katika kuinua Elimu ya Tanzania