
Tamasha la Kili Music Tour limekamilisha awamu ya kuzunguka mikoani kwa show iliyofana katika uwanja wa Mkwakwani Tanga. Tamasha hilo linalidhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager lilipambwa na burudani toka kwa wasanii wanaofanya vizuri nchini wakiongozwa na malkia wa mipasho Khadija Kopa na mfalme wa taarab Mzee Yusuph ambao waliongoza kundi la wasanii kumi kutoa burudani kwa wakazi wa Tanga.
Tamasha hili sasa linarejea jijini Dar es Salaam ambapo Jumamosi Septemba 6 litahitimishwa katika viwanja vya Leaders Club
Mtangazaji wa EATV Abdallah Hamis Ambuaa “Dulla” akiendesha shindano kwa kina dada wa Tanga waliojitokeza uwanjani kushuhudia Kili Music Tour
Umati wa mashabiki ukisubiria kwa hamu burudani uwanja wa Mkwakwani.
Backstage: Nikki wa Pili na Ommy Dimpoz
Backstage: Profesa Jay
Ommy Dimpoz ndiye aliifungua pazia la burudani Mkwakwani.
Richard Mavoko akiimba kwa hisia katika Kili Music Tour Tanga
Ben Pol mmoja ya wasanii walioshangiliwa sana katika usiku wa Kilimanjaro Music Tour akiwa jukwaani
Backstage: Joh Makini
Profesa Jay akichana moja ya nyimbo zake kali
Mkongwe wa Hip Hop Profesa Jay akisikiliza kelele za mashabiki waliokuwa wakiimba wimbo wake wa zari la mentali
Joh Makini toka Weusi akiwa jukwaan
Shabiki akionyesha bango la Weusi
Nikki wa Pili
DJ Choka akiwa kazini
Weusi wakilishambulia Jukwaa kwa pamoja
