
Karibia asilimia 80 ya maafisa wa polisi katika mji wa Parma kwenye jimbo la Missouri wamejiuzulu kazi zao za uaskari baada ya mwanamama mweusi kuchaguliwa kuwa meya wa mji huo.
Katika hali isiyo ya kawaida mwanasheria, mhasibu na afisa wa kutibu maji pia wamejiuzulu nafasi zao katika ofisi za umma mjini humo.
Mwanamama huyo Tyrus Byrd ambaye alikuwa mhasibu wa mji huo aliapishwa jana baada ya kumshinda meya wa mji huo Randall Ramsey aliyekaa madarakani kwa miaka 37.
Haijafahamika wazi sababu za mapolisi hao kuacha kazi japokuwa mpaka sasa sababu zilizo wazi zinaonyesha ubaguzi wa rangi kama sababu iliyochangia polisi hao ambao ni wazungu kuacha kazi.
Mji wa PARMA una wakazi 750 na polisi 6 amabapo watano kati yao wamejiuzulu na amebaki polisi mmoja.
