Drake ambae juzi kati ametoa tunzo zake zinazoitwa “Hood Grammy” repa huyo wa “0 To 100” anatakiwa ajibu shutuma ambazo zimetolewa na stripper wa Houston kuelekezwa kwa Drake kwamba alimtumia watu nyumbani kwake
wamtishie mwanadada huyo. Akieleza Jhonni Blaze amesema yeye na Drake walikuwa na mahusiano ya kimapenzi, lakini mambo yalikuwa mabaya na Drake kuchukia baada ya Blaze kutangaza kwa watu mahusiano yao. TMZ imeripoti kwamba polisi wa Houston rasmi wameanza uchunguzi na wanatarajia kuongea na Drake kuhusiana na swala hilo. Blaze alienda polisi kutokana swala hilo lakini bado hajaamua kuyashikilia kwa nguvu malalamiko hayo. Wazi kabisa Blaze pia amesema kwamba alipewa mimba na repa huyo, lakini upande wa camp ya Drake wamekana mashtaka hayo.