Wakati rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza kuunda serikali mpya, zimepatikana taarifa kuwepo kwa mwaliko kutoka ikulu ya Marekani kwa Rais Barack Obama akiwaomba Kenyatta na makamu wake Ruto kuhudhuria.
Chanzo kimoja chenye ukaribu na ubalozi wa Marekani nchini Kenya kimeuambia mtandao wa daily post kuwa Rais Obama ametuma barua za mwaliko kwa viongozi hao wawili Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto zikiwaomba kuhudhuria katika halfa ya chakula cha jioni kwa wakuu wa nchi za Africa itakayoandaliwa na ikulu ya Marekani baadaye mwaka huu.
Chanzo hicho kimeendelea kusema kwamba rais Obama alifurahishwa kwa jinsi uchaguzi wa Kenya ulivyomalizika kwa amani, na anahitaji kuwashukuru viongozi hao kwa kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi.