Rais Wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete Leo amewaapisha mawaziri saba na manaibu waziri 11 kati ya mawaziri 8 na manaibu waziri 13 aliowatewa Na kutangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni sefue
Mawaziri Pamoja Na Manaibu Hao wameapishwa Leo katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ikulu jijini dar es salaam.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jiji Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali akiwemo Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania Drk.Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mh.Minzengo Pinda, Naibu spika wa bunge Mhe. Job Ndugai, katibu wakuu na baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano ndugu na jamaa na marafiki wa viongozi.