LoadEyes Akiwa Mikononi wma police baada ya tuhuma za kuiba Lap top
Msanii Ray C ambaye amepona na kutoka katika kisima cha matumizi mabaya ya kulevya amemuasa mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki mwenzie kutoka Kundi La weusi LoadEyes kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa maana ndio yanayomfanya akumbane na majanga anayokumbana nayo kwa sasa
Ni week End Tu iliyopita Msanii huyo wa kundi hilo la weusi LoadEyes alikamatwa na kufikishwa lupango baada ya kutuhumiwa kwa wizi wa Lap Top, Kundi la weusi limetangaza kumsimamisha msanii huyo kwa muda kutokana na makubaliano yao ndani ya kundi lakini kikubwa ni kutokana na Msanii Huyo kujihusisha na vitendo haramu vinavyoweza kuchafulia kundi sifa
Kupitia ukurasa wake wa Insta Gram Ray C alimuandikia Ujume wa kumkanya na kuungana naye katika tiba ya kutoka katika dibwi jilo msanii huyo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani na ndio anayesemekana kumuingiza Ray C katika matumizi hayo mabaya ya madawa ya Kulevya