
Ukiwa kama mtu maarufu unakuwa unatazamwa kama wewe ni kioo cha jamii, kitu utakachokisema au kufanya watu wataiga au laah!!
The bad gal Riri ameendelea kushika headlines mbalimmbali duniani baada ya kupost tweet iliyoandikwa FREE PALESTINE na baada ya dakika nane baadae tweet hiyo ikawa imefutwa, ingawa Rihanna amesema hakutaka kutweet taarifa kutoka chanzo cha taarifa hii kiliiambia TMZ.
“Aliifuta kwa sababu hakutaka iwe tweeted na wala hakujua kama alitweet mpaka alipoanza kusikia kutoka kwa mashabiki wake” kilisema chanzo hicho. “
Chanzo hicho kimesema kwamba Rihanna alikuwa akisoma habari kuhusu mgogoro unaoendelea mashariki ya kati, anasema akagusa link hakujua kama imekuwa tweeted, ndipo alipoanza kupokea meseji zikimuuliza kwanini anachagua upande yeye akiwa ni mtu maarufu.
TMZ inakubali kwamba maelezo ya Rihanna yana walakini, kwa sababu mpaka mtu atweet atatakiwa aandike meseji au cut na kupaste kisha ubonyeze kitufe cha kutweet.
Kumekuwa na mgogoro kati ya Israel na Palestina kwa miaka mingi sasa, mgogoro ambao umeibuka tena tena mwezi huu kutokana na mauaji ya vijana watatu wa Kiisrael na mmoja wa Kipalestina. Taarifa kupitia CNN zinasema hakuna upande unaorudi nyuma kuacha mapigano toka Jumatatu Julai 14 idadi kubwa ya watu wameuawa Gaza.
