Kampuni ya Tanzania Top Modal Agency Limited imeandaa shindano la wanamitindo kwa lengo la kuibua vipaji vya wanamitindo pamoja na kuenzi mavazi na utamaduni mwa mtanzania.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo Jackson Kalikumtima akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam amesema kwamba shindano litaanza novemba mosi mwaka huu ambapo fainali zake zitafanyika siku ya uhuru wa tanganyika yaani Desemba tisa mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Amesema kwamba washindi wa shindano hilo watapigiwa kura na kuchaguliwa na wananchi kwa kushirikiana na timu ya majaji watakaohakikisha kwamba haki inatendeka.
Amesema kwamba washindi shindano hilo wataiwakilisha tanzania kwenye shindano la mitindo la dunia.