
Mkali wa ngoma ya “New Flame” Chris Brown hatofanya show kwenye nchi 2 mwezi huu,Mwezi Septemba haikuonekana kama Chris Brown angeweza kuruhusiwa kuingia Australia siku za hivi karibuni.
Serikali ya Australia ilimpa msanii huyo kutoka Virginia, Chris Brown notice ya makusudi kuingia nchini humo, ambayo itamzuia au kuwa na uwezekano wa kufanya tour yeyote kama ilitakiwa ifanyike.
Ukweli, promota wa tour hiyo amefuta tour hiyo ya Australia na New Zealand,taarifa za Billboard ziliieleza na kuandika maelezo kuhusiana na kufutwa shows hizo.
“Mr Brown na Promota wote bado wanamatumaini shows zitafanyika siku chache zijazo,Mr. Brown anatamani kuulezea shukrani zake za dhati kwa mashabiki kwa support na wategemee tour itakayokuwa ya mafanikio siku zijazo, Alisema promota wa One Hell of a Night tour.
Chris Brown alikuwa afanye tour yake Perth, Melbourne,Sydney na Brisbane kati ya Desemba 9 na Desemba 16.
Kosa lililosababisha Breezy akatazwe kuingia Australia ni baada ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake muimbaji Bad girl Riri Rihana, nchi nyingine ambazo zimemzuia Chris Brown kuingia katika nchi zao ni Britain,Canada na New Zealand.
