Kocha maarufu na aliyewahi kupata mafanikio makubwa nchini Uingereza Sir Alex Ferguson atastaafu kama kocha wa klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu huu.
Ferguson amefanikiwa kushinda mataji 13 ya Ligi kuu ya soka nchini Uingereza wakati wa uongozi wake wa misimu 26 katika klabu hiyo.
Klabu ya Manchester United imetoa taarifa rasmi leo iliyomnukuu Sir Ferguson akifafanua kuwa msimu huu wa 26 ndio utakaokuwa wake wa mwisho.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema ametafakari sana kuhusu uamuzi wa kustaafu kwake.