
Snoop Dogg aliulizwa kuhusu kufanya kazi na Iggy Azalea, lakini alijibu akimnukuu Big Sean “I don’t F….With You”.
Siku chache baada ya repa kutoka Australia Iggy Azalea naye aliulizwa kama hatawahi kufayna kazi na Snoop Dogg kufuatia tofauti zao zilizojitokeza siku za nyuma naye pia aliulizwa swali hilo hilo.
Alipofuatwa na TMZ katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, repa huyo kutoka California hakutoa jibu la ndio au hapana lakini alimnukuu Big Sean na E-40 “I don’t f…..wit you”
Na Iggy alipoulizwa swali hilo hilo alijibu akamuuliza aliyemuuliza swali kama wewe ndo ungekuwa mimi ungefanya?
Ugomvi mkubwa katika mitandao ya kijamii kati ya Snoop Dogg na Iggy Azalea imeonekana umefika mwisho mapema mwezi huu kufuatia maongezi ya simu kati ya Snoop na Boss wa Iggy T.I.
Kufuatia maongezi ya kwenye simu yaliyofanyika kati ya Snoop na T.I, Snoop aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa instagram.
“Nimetoka kuongea na mshikaji wangu TIP, Mfalme wa Atlanta na rasmi ugomvi umeisha, hakuna maongezi mabaya tena kati yangu na Iggy, naomba msamaha, Yeah, naomba msamaha, samahani, sintarudia tena” aliandika Snoop kwenye ukuraswa wake wa instagram.
