Kilimanjaro Tanzania Music Awards winning producer mkali Man Water a.k.a Man Maji kama wengi wanavyomfahamu, ametangaza kupandisha gharama za kurekodi wimbo moja kutoka gharama za sasa hadi kufikia milioni moja.
Amesema hayo kutokana na kwamba siku zimeenda na bei za kurekodi zimekuwa zile zile tu, huku wao watayarishaji wa mapigo ya muziki wakibaki wakiwa wamedumaa wakati wasanii wanafanikiwa kuliko wao, akasema hajafanya hayo kwa sababu ya wivu kwa wasanii ni kwamba ili uendele lazima ukubali mabadiliko katika maisha yako.
Ili ufanikiwe kuna vitu ambavyo untakiwa uchukue risk bila kuogopa nini kitatokea kama wasanii hawatakwenda kurekodi kwa sababu bei imepanda ni sawa lakini yeye anategemea ubora wa kazi anaoufanya kwa hiyo anaamini anaweza kuendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki.
Soko lolote linahitaji bidhaa bora na kama wewe mfanyabishara unaamini bidhaa yako ina ubora na soko huria unaweza kuweka bei unayotakamteja anayehitaji bidhaa bora atakuja kwako.
Wasanii watakaokuja na kufikia malipo hayo ya milioni moja atafanya nao kazi.