
Du hii suruali ya jeans ya Msanii Diamond Platinum sijui ni moja au anazo nyingi zinazofanana, Amekuwa anaonekana nayo mara kibao sehemu tofauti tofauti na siku tofauti tofauti, sehemu nyingine akiwa tu kitaa, au studio, sehemu za interview, viwanja vya ndege akisafiri hata katika shows pia ameonekana nayo
Kwa upande wake Diamond anapenda sana rangi nyekundu nyeusi na nyeupe kutokana na maelezo yake inawezekana basi kwa mtindo huo alinunua suruali hizi nyingi kwasababu ya sababu hizo au ndio Suruali aliyoona imekmaa Zaidi si unajua bwana hata wewe katika nguo zako kuna nguo huwa unaipendaaaaaaa…
Kupitia ukurasa wake wa Wa picha wa Instagram utagundua jinsi vazi hili katika suruali hii ya jeans nyeusi iliyochanika chanika bwana huyu amekuwa akiitupia sana katika nyakati tofauti tofauti.
Hapa tunapata Funzo ili upendeze si lazma uwe na manguo mengiiiiiiiiiiiiii la hasha unaweza kuwa na nguo chache ila ubunifu wa kubadilisha viatu kofia au hata mashati flana na tops zikakuanya uonekane ni mwenye viwalo kibao lakini zaidi kutokelezea si lazma uwe na rundo la nguo ile unayoiona inakutoa na upo confortable nayo unaweza cheza nayo na ukatoka bomba
MTAZAME HAPA AKIWA KATIKA KIVAZI HICHO BADALA YAKE AKIWA ANABADILI BADILI VIATU AU KOFIA AU FLANA NA MASHATI
PICHA KUTOKA UKURASA WA DIAMOND WA INSTAGRAM
