KAMPUNI ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezindua rasmi Siku ya Msanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Jumamosi 25 Oktoba 2014.
Mgeni rasmi katika “Siku Ya Msanii” alikuwa Makamamu wa kwanza wa rais Mhe. Dk. Ghalib Bilal, akiwemo naibu Waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo Mhe. Juma Nkamia amabe alito a hotuba kwa niaba ya Waziri wa michezo, utamaduni, vijana na michezo Mhe. Dk. Funellla Mukanagara.
Tuzo ya Msanii aliyejitolea Maisha yake yote maisha yake yote katika sanaaa alikuwa ni Edward Said Tingatinga, Josephat Kanuti alichukua tuzo ya msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini.
Kila mshindi wa tunzo hizo alipewa milioni 5 kila mmoja kutoka kwa mgeni rasmi Mhe. Dk Ghalib Bilal ikiwa ni hongera kwao kwa mchango wao mkubwa katika sanaa ya Tanzania.
Siku hiyo ilipambwa kwa burudani maridhawa kutoka kutoka Diamond platinumz, Yamoto Band, Wana Njenje Band, Vikundi wa ngoma mbali mbali, sarakasi na mitindo.
Washerehesahji walikuwa ni Jokate Mwegelo na Chriss Mauki.