Moto mkubwa uliozuka katika ghala ya kuhifadhia bidhaa kwenye jengo ka Millenium Businness Park Jijini Dar Es salaam ulisababisha wafanya biashara waliokua wakimiliki bidhaa hizo kuangua vilio.
Bidhaa zilizoteketea ni pamoja na Mipira ya Baiskeli, Vyombo vya Udongo, chupa za chai, Sabuni za unga, pedi na vigae vya Sakafuni za kampuni ya Sunda International na mitanbo au zana za kisasa za ulinzi zilizokua zinamilikiwa na kampuni ya Hawk Security System Ltd.
Chanzo cha Moto huo inasemekana ni hitilafu ya umeme iliotokea ndani ya jengo hilo
Kikosi cha zima moto kilifika katika eneo la tukio kuzima moto huo huku baadhi ya wananchi wakiwatupia lawama mbali mbali lakini pia wananchi wengine waligeuzia kibao wamiliki hao kuwa hawana mpangilio mzuri wa bidhaa zao katika maghala yao hivyo inaleta ugumu pindi maafa yajitokezapo.