Mwanaume mmoja wa ki Mexico Jose Salvador Alvarenga amenusurika kifo baada ya kupotelea katika bahari ya Pacific kwa zaidi ya mwaka mmoja
Jose Salvador Alvarenga aliokotwa pembeni ya bahari baada ya mawimbi ya bahari kumsukuma ufukweni ikiwa ni miezi kumi na tatu tangu aingine baharini karika kazi yake ya kutafuta samaki akitarajia safari yake ingekuwa ya siku moja tu lakini mambo yakawa ndivyo sivyo
Watu wengi wamebaki na maswali mengi kama mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 37 aliwezaje kuishi baharini kwa kipindi chote hicho akiwa ndani ya kiboti kidogo tu.
Lakini Bwana Alvarenga alisema aliweza kuishi kwa kunywa maji ya ngisi na mkojo wake huku akila vijisamaki vibichi alivyokua anavitega kwa mikono yake
hata hivyo Binadamu huyo mwenye bahati ya ajabu alionekana ni mwenye afya nzuri tu japo alikuwa anaonekana mchovu sana na sasa yupo katika hospital akiangaliwa afya yake kitaalam zaidi
Wakati anaondoka kabla ya kupotea alikuwa na mwenzake ambaye yeye alifariki baada ya miezi 4