Rihanna hajawahi kuwa na aibu juu ya kuonyesha maumbile yake lakini kwa kipindi hiki amekuwa kwenye midomo ya watu wengi duniani pale alipotokea kwenye red carpet ya Council of Fashion Designers Awards Jumatatuiliopita.
Nguo aliyokuwa amevaa unaona kila kitu , nguo hiyo ilikuwa ni noma sana . Rihanna pia alionekana kwenye jarida la Kifaransa la Liu akiwa na pozi zake hizo hizo za uchi uchi.
Wanamuziki wa siku nyingi wa kundi la TLC hawajavutiwa kabisa na kitu anachofanya Rihanna kwa sasa wakati wakipiga story na kipindi cha Sunrise Morning nchini Australia ambako kwa sasa wako huko wakifanya show zao zenye mafanikio.
Wasanii hao ambao wameshawahi kushinda tuzo za grammy TLC walimrekebisha Rihanna kwa kutumia kukaa kwake uchi ili afanye vizuri katika muziki.
Walisema wao walifanya vizuri siku za nyuma hata mpaka sasa lakini bila kukaa uchi tungeweza kwenda kila mahali tumeachia matiti yetu nje ni rahisi kuuza ngono lakini hatuwezi kusema chochote zaidi kwa sababu watu watakuja watasema ooh sijui TLC wanamuonea wivu Rihanna.
T-Boz na Chili wameona Rihanna anavyofanya sio fresh.
Rihanna hakukaa kimya baada ya mashambulizi hayo ya maneno badala yake aliwajibu kwa nia yake kwa kubadili twitter header yake akaweka picha ya TLC enzi zao wakionekana hajavaa nguo za juu lakini wamezui sehemu ya vichuchu, TLC walionekana wanapoint ya msingi lakini Rihanna akaamua kuwashushua na kuwafanya waonekane kama wanafki.
Rihanna aliandika kwenye ukurasa wake wa tweet
“When there’s no changing the fact that I’m me, and they’re well..they’re them”
TLC wamejishau na wao walishafanya kitu kama hicho lakini hakikuwa na impact kubwa labda ni sababu social networks hazikuwepo kipindi kile .