
Mkurugenzi wa kampuni ya benchmark production inayoandaa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search Rita Poulsen akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza kuwaingiza washiriki wake walioingia 20 bora kambini, ambapo pia amesema litakuwa likionyeshwa na kituo cha televisheni cha TBC kila Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa kila jumatano saa nane mchana.
Pia Amesisitiza kuwa wamepata washiriki mahiri kutoka mikoa mbalimbali, hivyo mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkali sana na anaamini watapata wasanii bora zaidi kuliko miaka iliyopita. Anayefuata ni Meneja TBC 1 Edna Rajab, Mshindi wa BSS 2012 Walter Chilambo na Arnold Madale wa Zantel.
Meneja TBC 1 Edna Rajab akifafanua kuhusu kituo chao cha televisheni kuonyesha mashindano ya mwaka huu ya Epiq BSS ambapo amesema ni furaha kwao kufanya kazi na BSS na kuwaahidi watazamaji kuona kipindi hicho bila matatizo yeyote.
Usaili wa Epiq Bongo Star Search kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.
Washiriki 50 walipatikana kutoka mikoa yote na wamechujwa na kubaki washiriki 20 ambao ndio watakao ingia kambini.
Washiriki wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.
