Mwanamitindo ambae alichukua nafasi ya pili ya pili katika Shindano La Miss BumBum huko Brazil, mwanadada huyo ameweka wazi madhara yaliyomkuta baada ya kufanyiwa upasuaji na kutengenezwa shepu yake ili aweze kuwa na muonekano mzuri.
Andressa Urach mwenye miaka 27, alitumia muda wa mwezi mmoja katika chumba cha watu mahututi na aliogopa kupoteza mguu wake baada ya sehemu alizofanyiw upasuaji na kuwekea vitu kuanza kuozesha misuli na vitu hivyo vilivyojazwa vilitakiwa viondolewe katika mwili wake, ili kuondoa sehemu hizo zilizokuwa zimedhurika na kutishia maisha yake.
Picha zinazoonekana zikionesha jinsi Urach alivyoathirika kutokana na upasuaji huo wa kutengeneza umbo lake kwa kuongeza mapaja na makalio, Brazil imeipita U.S. kwa kufanya masala haya ya urembo wa kufanyiwa upasuaji.
Miss Urach anasema ameshwahi kufanya mapenzi na Cristiano Ronaldo, na amsema ameshashawahi kufanya upasuaji kama mara nane katika miaka minane iliyopita.
Upasuaji huo unahusisha pua, uso kurekebishw, taya na kuongezwa matiti, lips na hata kupunguza mashavu ya uke.
Miss Andressa Urach Kabla Kabla hajapatwa na madhara
Nchi ya Brazil imeizdi Marekani kwa mwaka 2013 na kuwa ndio nchi ambayo kwa kiwango kikubwa watu wake wamekuwa wakifanya surgery kuliko nchi yeyote Duniani
Angalau Surgery 1.5million zilifanyika huko America Ya kusini ambapo kulikuwa na ongezeko la 600,000 ndani ya miaka 2 tu
Surgery Hizo Zinajumuisha za matiti kwa kiwango cha 226,000 na 64,000 za upasuaji wa Makalio na mapaja kidunia
Brazil Ina zaidi ya upasuaji wa aina hiyo 5,000 ambapo ndani yake upasuaji uliofanyika ni zaidi ya 78,000 ukijumuisha Pua upasuaji 77,000 na 219 ukiwa ni upasuaji wa sehemu za siri kwa mujibu wa International Society of Aesthetic Plastic Surgeons.
Mwenza Wa Mrembo Huyo Aliyekumwa na Maswahiba hayo Jessica Lopes ambaye alishare shape yake akiwa flat pamoja na miss Urach alisema mwaka jana kuwa ‘Adressa Na mimi tutakwenda kwa ajili ya Upasuaji kama tunakwenda Dukani tu, Wakati mwingine tulikubaliana kwenda kwa ajili ya upasuaji pamoja’ hatukuogopa.Tulikuwa Watumwa wa Urembo”