
WATANZANIA TUMEANZA VIZURI MCHEZO WA BIG BROTHER BAADA YA MUWAKILISHI WETU FEZA KUWA MSHINDI WA KUINGOZA JUMBA HILO KATIKA WIKI YA KWANZA TU BAADA YA MCHEZO WA KUTAFUTA BOX LENYE USHINDI KATIKA BUSTANI NA KUWASHINDA WENZAKE.
AKIWA KAMA KIONGOZI WA NYUMBA HIYO FAIDA KUBWA ZAIDI NI KUJINASUA KAMA ANAWEKWA KATIKA KIKAANGO CHA KUNG’OKA KATIKA KUPIGIANA KURA ZA MTOANO…. NA KAMA YEYE HAYUPO ANAPATA KIBARUA KIGUMU KIDOGO CHA KUMPENDAKEZA MTU ALIYEKO KIKAANGONI NA KUMEWEKA MBADALA WA MTU AMBAYE HAKUPIGIWA KURA KABISA, HAPO NDIO MSALA UNAPOANZA KWA MAANA YA KUTENGENEA BIFF KATI YA ALIYEWEKWA MBADALA WA MWENZIE KATIKA WIKI YA MTOANO… KIBARUA KINAKUWA KIGUMU ZAIDI SIKU YA MTOANO AMBAPO KIONGOZI ITAMBIDI ASEME KWA WENZIE MAAMUZI ALIYOYAFANYA HUKO KATIKA CHUMBA CHA MAONGEZI NA KAKA MKUBWA ‘DIARY ROOM”
PAMOJA NA CHANGAMOTO HIZO ZA UONGOZI LAKINI PIA KIONGOZI ANA NAFASI NZURI YA KUWASOMA WENZIE KUTOKANA NA KUPEWA MAMLAKA YA KUWAONGOZA KWA JINSI INAVYOTAKIWA
FEZA ALI MSAVE MSHIRIKI KUTOKA GHANA ELKEM NA KUMEWEKA KIKAANGONI MDADA BETTY WA ETHIOPIA HUKU WASHIRIKI WENGINE WALIO KIKAANGONI NI PAMOJA NA HUDDAH KUTOKA KENYA, DENZEL KUTOKA UGANDA, SELLY KUTOKA GHANA, NATASHA WA MALAWI NA BETTY WA ETHIOPIA ALIOTOLEWA KAFARA NA MKUU WA NYUMBA FEZA KUTOKA TANZANIA
