Mtu mmoja ambaye alikufa baada ya kupiga shots za kutosha za vodka akiwa na marafiki alianguka na kupelekwa mochwari kabla hajaamka.
Baada ya kula bata sana akiwa na marafiki alizimika na marafiki ndipo walipoita gari la wagonjwa (Ambulance) nyumbani kwao huko Khasanky huko mashariki ya mbali Urusi. Gari la wagonjwa lilipo wasili ilishatangazwa kwamba mtu huyo ameshakufa na walimchukua na kumpeleka mochuari.
Wakiaongea na waandishi wa habari wa eneo hilo la Khasanskye msemaji wa polisi Aleksey Stoyev alisema
‘Usiku ule mochuari ilikuwa imejaa kupita uwezo wake, miili ilikuwa haijawekwa tu kwenye shelfu lakini ilikuwa imelazwa kwenye sakafu katika chumba cha mafriji, sehemu ambayo hata mtu huyo aliyesemekana kufa aliwekwa, aliamaka kabla ya kuanza kutafuta mlango wa kutoka ambapo aliwaogopesha sana wafanyakazi, katika hali ya kutofahamu mtu huyo aliamka na kushindwa kujua alikuwa wapi, akiwa kwenye giza alihisi mtu mwingine akiwa pembeni yake wabaridi kabisa kwenye mikono yake kwa uoga alikimbilia mlangoni, baada ya hapo alirudi kwenye party, aliwaona rafiki zake bado wanakunywa lakini hapa sasa akiwa anajielewa’ alisema msemajihuyo wa polisi.
Baada ya kuwaambia marafiki wake waliokuwa wameshtuka sana kilichotokea kule mochuari, party hiyo ilihamia kusherekea na kusherekea kufufuka kwake, re-birth party.
UK Mirror.