Shabiki mmoja wa mpira ameshtakiwa kwa kosa la kumchinja mke wake na watoto wawili kabla hajaelekea kuangalia mechi ya kombe la dunia katika bar wakati ilipocheza mechi ya kati ya Uingereza dhidi ya Italia.
Raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 31 anaeitwa Carlo Lissi kwa sasa anatuhumiwa kwa mauaji ya watu watatu ambao ni Cristina Omes na wasicha wawili mmoja ana miaka 5 na mwingine ana miezi 20 walikutwa nyumbani kwake wakiwa wamekufa karibu na Milan mapema Jumapili iliripoti UPI.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 38 alichinjwa wakati akiangalia TV akiwa kwenye kochi kabla ya Lissi ajawashambulia watoto wake wawili waliokuwa wamelala. Mtu huyo baada ya kumaliza mauaji akatupa silaha kwenye shimo na kuelekea bar mida ya saa 5:30 usiku, Polisi waliiambia The Mirror.
Mida ya saa 2 usiku Lissi alirudi nyumbani na katika hali ya kushangaza iliripotiwa kwamba alikataa na miili yenye damu ilikuwa tayari polisi, baada ya saa chache baada ya mahojiano alikiri kufanya hivyo.
Mtu huyo aliwaambia polisi kuwa alikuwa akimpenda mtu mwingine na ilikuwa hakuna njia ya kuacha kumpenda. Lissi anasubiri mashtaka ili ahukumiwe kwa ajili ya kuua familia yake kwa kuwachinja.
Siku hiyo Italia ilishinda 2 – 1 dhidi ya Uingereza.