Jimmy Winfrey amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 20 baada ya kukutwa na makosa ya kushambulia tour bus la Lil Wayne mwezi Aprili mwaka huu, taarifa kutoka Bossip zimeeleza.
Makaratasi yaliyowakilishwa Desemba 18 zinasema Winfrey alikuwa akipinga hukumu hiyo, mwezi Novemba Winfrey alihukumiwa miaka 10 jela na miaka 10 chini ya uangalizi kwa makosa 6 ambayo yote yalihusu uhalifu.
Young Thug na Birdman walitajwa kuhusika lakini hawakushtakiwa, Winfrey alijaribu kufanya kesi hizo zitupiliwe mbali kwa sababu rappers hao hawakushtakiwa na kwa sababu alisema mashtaka hayakuwa na ushahidi ulionyooka.