Amber Rose hana uhakika kama mashoga watawahi kukubalika au hawatakubalika ndani ya Hip Hop, Alitoa maoni hayo wakati akipiga stories na Vlad TV , Amber Amesema kwani hao ambao wameingia katika Hip Hop waliingia kama wasaidizi na kwa ajili ya kuwapangia nguo wasanii kuhakikisha wanakuwa na muonekano mzuri wanapokuwa mbele ya mashabiki yani stylists.
“Nadhani inaonekana wanakubaliwa zaidi sasa hivi na pia nitakwambia kwa nini, kwa sababu mashoga wanajua fasheni, wanajua kitu kinachofanya vizuri kwa muda huo, na marepa wengi stylists wao ni mashoga na wasaidizi wao ni mashoga pia, ndo kama hivyo, wanafanya kazi nzuri, sijali kama wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja au vipi nadhani tunasonga mbele” Alisema Amber.
Mwanamintindo huyo ambae ameolewa na Pittsburgh Pennsylvania Lyricist Wiz Khalifa alifunguka hayo baada ya kuulizwa kama mashoga watawahahi kukubalika katika Hip Hop, Akasema ni mafanikio itakuwa fresh lakini hakuna uhakika jinsi walivyochukulia kwa pande zote, mashoga na Jumuiya ya Hip Hop.
“Sina uhakika, hilo litakuwa jambo fresh,nadhani itakuwa fresh, nasijui jinsi gani jamii ya kishoga itakuwa nao pia” alisema Amber Rose.
Akielezea mahusiano yake na mashoga katika jamii Amber Rose amesema amekuwa na watoto mashoga wengi akiwa mdodo na pia huwa anajiachia watu waliojibadilisha jinsia zao sehemu mbali mbali huko New York.
Yeye anaona haina tatizo ili mradi kazi inafanyika fresh kila mtu na maisha yake.