
Amber Rose anaonekana kutweet kuhusu hisia zake juu ya talaka ambayo ipo njiani kutoka kwa Wiz Khalifa
Amber Rose alitweet mara 2 siku ya Jumatatu Oktoba 6 kuhusu kinachotokea kuwa kama baada ya majanga ya kutaka talaka kutoka kwa Wiz Khalifa.
“Muda wa asubuhi ni wakati mgumu sana” tweet ya kwanza aliandika hivyo.
“Maumivu, naamka kila asubuhi nahisi kama rafiki yangu kipenzi kafa, sikujua maana ya maumivu ya kweli yalivyo mpaka kipindi hiki” tweet ya pili ya Amber Rose aliandika.
Mwezi uliopita Amber Rose alitaka talaka kutoka kwa mume wake mkali Wiz Khalifa kutokana tofauti ambazo haziwezi kurekebishika.
Katika stori iliyotoka Oktoba 1, redio ya New York Hot 97 na mtangazaji wa kituo hicho Peter Rosenberg alisema Amber Rose alimkamata Wiz Khalifa akimdanganya na mapacha waliokuwa wakitumia nyumba moja.
Wiki tatu tu zilizopita Wiz na Amber kupitia instagram yao walikuwa wakisherekea mapenzi yao kwa kila mmoja wao na vitu kama hivyo, ilikuwa nyumbani.
Imeripotiwa Amber Rose atapewa dola milioni 1 kutoka kwa Wiz Khalifa na hii ikiwa ni makubaliano yao kwa ajili ya mtoto wao Sebastian.
Sasa hivi mahusiano ya mastaa yamekuwa yakiyumba sijui tatizo ni nini…lakini muda mwingine wanatafuta kick kwa ajili ya biashara wanakuwa wakitafuta attention lakini ukichunguza unakuta hakuna ishu yeyote.
Amber Rose na Wiz Khalifa inasemekana wanaachana kwamba talaka inakuja lakini hakuna kitu, hayo ndo maisha ya kicelebrity.
