Taarifa kuwa dereva wa taxi nchini Afrika Kusini alikufa kufuatia tukio la kufungwa pindu kwenye gari la polisi na kuburutwa mitaani.
Polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi kubainisha ukweli wa tukio hilo ambalo limetokea katika mji wa Daveyton mashariki mwa jiji la Johannesburg
Taarifa za awali kutoka katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini zilisema kuwa polisi walimfanyia ukatili dereva huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Msumbiji, wakimtuhumu kuegesha gari lake vibaya
Picha za video zilizochukuliwa kwa kutumia simu ya mkononi, zilionyesha umati wa watu ukiangalia, huku maafisa wa polisi wakimfunga mtu huyo kwenye gari na kuondoka kwa kasi, wakimvuta barabarani.Inaaminika kuwa mtu huyo alikufa baadaye akiwa kizuizini.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekilaani kitendo hicho akisema hakikubaliki