Utafutaji mkubwa unaendelea pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya mtoto mwenye umri wa miaka 5 Ashya King aliyekuwa na uvimbe katika ubongo wake ambaye alitoroshwa na wazazi wake kutoka wodini bila idhini ya madaktari.
Hali ya mtoto huyo ipo katika hatari kutokana na kulishwa kwa kutumia mrija unaotumia betri ambayo muda wakeunakaribia kuisha. Police kutoka jimbo la Hampshire wanasema suala kubwa wanalolipigania ni maisha ya mtoto huyo ambaye anahitaji uangalizi mkubwa wa kitabibu. “Muda unakwisha” alisema msaidizi wa polisi konstebo Chris Shead, “Ni muhimu kuhakikisha kuwa Ashya anapatikana leo, asipopatikana hali yake itaathirika sana”.
Wazazi wa mtoto huyo ni waumini wa dini ya Mashahidi wa Yehova ambao hawakubaliani na matibabu yanayohusianisha na kuwekewa damu, kamera za hospitali zilionyesha wazazi hao Brett King na Naghemeh King wakimtorosha mtoto huyo kutoka hospitalini hapo.