
Kufuatia kufukuliwa kwa mwili wa mrehemu FARAHAN MALULI uliokuwa umezikwa ndani ya nyumba ya makazi maeneo ya Sharif Shamba manispaa ya ilala jijini Dar es salam, hatimaye mwili huo umezikwa leo na ndugu wa marehemu.
Imeshuhudiwa mwili huo ukiagwa na ndugu, jamaa na marafiki huku baadhi yao wakielezwa kusikitishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa marehemu.
Baba mzazi wa marehemu ABSALOM MALULI ambae amelishukuru jeshi la polisi kwa juhudi kubwa walioifanya tangu siku ya kwanza waliyotoa taarifa ya kupotelewa kwa mwanawe hadi alipokuja kupatikana akiwa ni marehemu.
Nae Mke wa marehemu TATU ALLY akizungumza kwa uchungu ameeleza jinsi alivyopoteza mawasilino na mumewe hadi kufikwa na umauti. Mumewe aliondoka ilikuwa tarehe 12 mwezi wa 6 2014 siku ya Alhamisi alipomuaga mke wake anakwenda kazini kuanzia hapo ndio hakurudi tena.
Marehemu FARAHA MALULI alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwezi Juni mwaka jana na mwili wake ulifukiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mtuhumiwa wa mauaji hayo HEMED HAMIS.
