Mwaka 2015 umeanza vizuri kwa msanii kutoka Kenya na msanii kutoka nchi jirni ya Tanzania, ambapo Avril kwa sasa anatengeneza kitu mahsusi kwa mashabiki wake akiwa na msanii mkali kutoka Tanzania mkali wa ngoma ya “Baadae”. Mkali Ommy Dimpoz.
Katika mitandao ya kijamii wikii imepambwa na picha na wasanii hao wawili wakionekana wakiwa na wakati mzuri pamoja wakisem ni maandalizi ya wimbo wao mpya ambao umewachukua miaka mitatu kuikamilisha.
Lakini ingawa tunafanywa tuamini tunachoambiwa na wanaotupa burudani, lakini mwenyewe unaonaje muunganiko wa Avril na Ommy Dimpoz?
Picha nyingi zimeonekana wakiwa saloon na sehemu mbali mbali kwa hayo tu yanatuambia kitu zaidi.
Lakini usichanganyikiwe, wawili hao wanafanya kazi tu kwa ajili ya wimbo wao ambautatoka muda sio mrefu.
Kitu kimoja ambacho na uhakika nacho ni kwamba ngoma hiyo itakuwa hit song. Ommy Dimpoz ni kama Diamond huwa haharibu pia Avril, kwa hiyo tusubiri colabp kutoka kwa Avril na Ommy Dmpoz.