Baada ya mkali wa ngoma ya “we belong together” Mariah Carey kuachana na mume wake, jamaa aliyekuwa katika kipindi cha TV kinachojulikana na “America’s Got Talent”, Nick Cannon, Mariah Carey alionekana akitumia muda mwingi sana akiwa na director Brett Ratner na kuwafanya mashabiki wake kushangaa na kusema wawili hao ni wapenzi.
Taarifa za In Touch Magazine zimeripoti Jumapili kuwa Mariah Carey na director Brett Ratner.
Kwa sasa Mariah Carey anatafuta furaha tu hakuna lingine, Huyu mpenzi wake wa sasa hivi Brett Ratner ana miaka 45, nadhani hapa Mariah Carey atleast amekutana na mtu wanaendana, Nick Cannon alikuwa ni mdogo sana kwake, ndo maana hata baada ya kuachana Nick Cannon alitoa sababu za kuachana na Mariah akasema anapenda muda wote atakachokisema aseme yes, yes, yes nah ii ni kwa sababu alimuona ni mdogo.
Taarifa za Jumapili zilisema kwamba Ratner alitengeneza video nyingi za Mariah Carey kuanzia albamu zake za mwanzo na aliendeleakuwa rafiki yake mkubwa hata wakati Mariah Carey alipokuwa na Nick Cannon. Kwa sasa sio Mariah Carey wala Brett Ratner amethibitisha hili.
Lakini kama hujui kusoma hata picha huoni? Taarifa zinaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa wawili hawa wanatoka, na vyombo vya habari duniani vimeripoti eventually Mariah Carey had found her happiness.