Msanii Matonya amekamatwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliopo manispaa ya Songea mkoani ruvuma.
Taarifa zinadai kuwa Matonya aliingia ukumbini akiwa amelewa, hali iliyomfanya ashindwe kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi huo baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo…
Baada ua hali hiyo, waandaaji wa show hiyo waliamua show hiyo ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni kununua bia .
Mbali na sakata hilo, Matonya alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam ….
Baada ya kuvuja taarifa hizo , waandaji walimfuata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu nyingine. …
Walipomkosa, waliamua kumvizia katika stendi ya mabasi ambako walifanikiwa kumkamata akijiandaa kusepa..!!!
Hadi sasa, msanii huyo yupo mahakama ya mwanzo …