MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu.
Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo,mwandishi wetu alilazimika kuwatafuta ndugu zake ili kuujua ukweli
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu yake, Binti kiziwi hajanyongwa bali ametupwa jela miaka mitano.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
DEMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo.
14 Comments
watu wanajihngiza ktk biashara haramu ya madawa ya kulevya kutokana na mfumo mbaya wa uchumi na wimbi la wimb la viongoz wasio waadilifu.hvyo ni wakat sasa wa serikal na jamii kwa ujumla kubadili mifumo yotdm ya usimamiz wa nch ya tz.ni aibu na hasara kubwa jtwa nch
PHILIPO
wanafikiri utajiri unatokana na unga tu wangalie mbinu nyingine ya kupata pesa
warudi vijijini wakalime mahindi wasikimbilie kifo shauri yao
ee mola turehemu vijana tutakwisha kwa umaskini nanyi wazazi mnaofurhia visa vy wenenu mnafatilia safari hizo au ndo wanapokamatwa mnaangua vilio?
PESA NZURI NI HILE UNAYOITAFUT KIHALALI NASI KISHETANI KAMA WAFNYAVY WENZETU,HAKUNA ASIEPENDA KUWA NAMAISHA MAZUTI BUT C KWAKUUZ MADAW NAKUTEKETEZ WENGINE ONA SS MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI.
Nikwelihiyo ni tamaaya maisha mazuriAdd Your Comment
Jaman mbna mnatutia aibu TANZANIA?
Haitoshi kukamatwa kwa hao wabebaji pekee,bali watafutwe na hao mapapa wanaowapa hiyo dili.
Kiukweli biashar ya madawa ya kulevy inawaadhili vijana weng hap tanzania!hivyo ni vizuri mataifa yot kushirikiana na wa2 wanosambaz hay madaw!!!
Add Your Comment
HERI YA SHETANI UNAE MJUA KULIKO MALAIKA USIE MTAMBUA, watu wanashindwa kuelewa kuwa wambili havai moja na mafanikio yanakuja kwa kujituma kihalali na sio kutumiwa na mtu ili upate mafanikio,ukiwauliza wote hao waliokamatwa na madawa ya kulevya utakuta wametumwa na watu wengine.HII NI MITANDAO YA WAKUBWA TUSIDANGANYANE MIMI NA WEWE KAMWE HATUWEZI KUFANYA HII BIASHARA,
sasa tuwasaidiaje wajameni, bora warudi kijijini tushirikiane kuendeleza kilimo
kwanzaaaaaaaaaaaaaaaaa
hali ktk madawa ya kulevya ni mbaya sana